MAELEZO MAFUPI KUHUSU SKAUTI ………………………………………………………………………………………………………………………. Skauti ni chama cha hiyari cha kielimu kinachotoa mafunzo kwa vijana wote bila ya ubaguzi wa rangi,jinsia,dini wala kabila. Skauti ilianzishwa mwaka 1907 huko nchini uengereza katika kisiwa cha Brown sea na major wa jeshi BADEN PWELL.

MALENGO YA SKAUTI

Malengo ya skauti ni kumuendeleza kijana kimwili,kiakili,kimtazamo,kijamii na kiimani ili kumfanya kijana aweze kujitegemea,kusaidia jamii na mwenyekuwajibika na mtu wa kufaa siku zote. Lakini lengo kubwa ambalo ndio linajumuisha malengo yote hayo ni kuitengeneza dunia kuwa bora,tukisema kuitengeneza dunia kuwa bora hatumaanishi kujenga magorofa au kuwa na majumba mazuri hapana ila tunaposema dunia kuwa bora ni kumjenga kijana katika maadli mazuri yanayompendeza mungu na jamii maadili ambayo kijana yatamfanya awe mtu wa kufaa sikuzote,awe mfano bora wa kuigwa katika maisha yake ya kila siku,katika kujitafutia rizki ya halali kila siku na awe balozi wa kuelimisha jamii mambo mazuri kaika uhai wake.

Ebu ujiulize wangapi leo hii wameondoka duniani lakini wameshindwa kuiacha dunia ikiwa bora,wamewaacha watoto wao wakiwa wahuni,wazinzi,wezi na hawafai kuigwa kitika jamii na wameshindwa kuwa mabalozi wa amani. Mimi,wewe na Yule ndio wakuiengeneza dunia kuwa bora kuliko ulivyoikuta.

NJIA ZA KUYAFIKIA MALENGO HAYO

Kuna njia sita (6) za skauti za kuyafikia malengo hayo:-

I. Ahadi na kanuni za skauti II. Mfumo wa vikosi vya watu sita mpaka nane III. Mafunzo endelevu IV. Mafunzo kwa vitendo V. Maisha katika uhalisia VI. Mahusiano ya vijana na watu wazima.



CREATING A BETER WORLD SCOUT SECTION

Kwakuwa skauti ni chama ambacho kinaowa elimu kwa vijana na ukizingatia kujana ndio mjenzi mkuu wa taifa na dunia hivyo akipotea ni hasara kubwa katika jamii basi skauti haikumuacha kijana yeyote ambaye anaelewa baya na zuri.


MIAKA 5-11_CUB SCOUT

Kijana mwenye umri wa miaka 5 hadi 11 huyu anaitwa cub scout na sanasana huwa ni wanafunzi wa shule za msingi,kijana huyu huwa analelewa vuizuri na hana mafunzo magumu na mwalimu wa skauti anaye mfundisha kijana mwenye umri huu huwa anaenda kozi maalum ya vijana hawa wadogo Kama unavyojua kumlea motto mdogo ni kazi ngumu sana.

MIAKA 12-15_JUNIOR SCOUT

Kuanzia miaka 12 hadi 15 na huyu anaitwa junior scou na hawa sanasana huwa ni wanafunzi wa sekondari na mafunzo yao ni tofauti na cub scout.

MIAKA 16-18_SINIOR SCOUT

Kuanzia miaka 16 hadi 18 na hawa huitwa senior scout sanasana huwa ni wanafunzi wa sekondari,form five.hawa mafunzo yao ni magumu na ufundishwa mambo mbalimbali ya kimaisha ikiwemo kundaa miradi amboyo baadae iamsaidia.

MIAKA 19-26_ ROVER SCOUT

Hawa sana huwa ni wanafunzi wa form five,six na chuo na huandaliwa kuwa viongozi wa na walimu wa skauti.

UONGOZI WA SKAUTI TAIFA

I. Rais wa skauti ni Waziri wa elimu wa kipindi husika. II. Mlezi wa skauti ni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wa kipindi husika. III. Wazamini wa skauti mh.ALLY HASSAN MWINYI na SALIM H.SALIMU IV. Washauri shekh mkuu wa Tanzania na askofu mkuu wa Tanzania V. Skauti mkuu wa Tanzania VI. Kamishna mkuu wa skauti Tanzania . VII. Makamishna wa mikoa VIII. Makamishna wa wilaya IX. Watendaji.


BE PREPARED

KAMBI,SAFARI NA SHEREHE ZA SKAUTI

Katika skauti kuna kambi za skauti ambazo zinaweza kuwa za mafunzo au za kielimu na kambi hizo zinaweza kuwa ndani ya mkoa,nje ya mkoa au nje ya nchi na kambi au safari hizo huwa mara mbili kwa mwaka yaani likizo ya muhula wa kwanza na likizo ya muhula wa pili.

Lakini pia kuna sherehe za skauti ambazo kila mwaka hufanyika,sherehe hizo ni

I. Kumbukumbu ya muanzilishi wa skauti- hufanyika kila mwaka ifikapo mwezi wa pili na hufanyika duniani kote. II. JOTAJOTI-jamboree onthe air and jamboree on the internet- hufanyika kila mwezi wa kumi kwa kila mwaka na hufanyika duniani kote. III. Tamasha la skauti ambalo hufanyika kila mwaka chuo kikuu lenye lengo la kuwasaidia waishio kwenye mazingira magumu.


……………………………….

MRATIBU MAFUNZO (W)KINONDONI