Rushwa na athari zake

edit

Rushwa[1] ni fedha au kitu cha thamani kinachotolewa na kupewa mtu mwenye madaraka ya jambo fulani ili mtoaji apate upendeleo Au Ni kwenda kinyume na mamlaka uliopewa kwa ajili ya mafanikio yako binafsi.Rushwa, kwa ufupi, ni adui wa maendeleo katika jamii yoyote. Ni janga linaloathiri taasisi za umma, sekta binafsi, na hata maisha ya kila siku ya watu. Kwa kuelewa kina na madhara yake, tunaweza kufahamu umuhimu wa kupigana dhidi yake kwa nguvu zote.

Kuna Aina za rushwa ambazo watu hutoa kwa ajili ya kupata upendeleo toka kwa wale wanaopewa ambao ni watu wenye mamlaka fulani juu ya jambo fulani ambayo mtoaji rushwa analihitaji.Rushwa imegawanyika katika makundi mawili nayo ni 1. Rushwa ndogo 2. Rushwa kubwa.

Kuna Aina nyingi Sana za rushwa[2].

  • Fedha
  • Mapenzi
  • Vyeo
  • Ahadi.

Athari za rushwa-

  • Kuzorota kwa kazi
  • Kushuka morali ya kazi
  • Kukosekana kwa haki
  • Huathiri misingi ya utawala bora,utawala wa kisheria na demokrasia.
  • Husababisha mgawo usio sawa wa rasilimali za Taifa.
  • Husababisha kukosekana kwa haki.
  • Wananchi kukosa imani na Serikali yao.
  • Huleta matabaka ya walionacho na wasionacho.
  • Serikali kushindwa kutekeleza miradi yamaendeleo.
  • Husababisha vifo.

Kila mwananchi ana wajibu wa kushiriki katika kuzuia na kupambana na rushwa kwa kufanya yafuatayo;[3]

Kutoa taarifa: Kila mwananchi ana jukumu la kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kwa TAKUKURU au kwa vyombo vingine vya sheria au dola. Taarifa zinaweza kutolewa kwa njia ya simu, barua, barua pepe au kufikisha taarifa hizo katika ofisi ya TAKUKURU Makao Makuu au ofisi zilizopo mkoani na wilayani kote nchini.

Kutoa ushahidi: Kutoa tu taarifa bila kuwa tayari kutoa ushahidi hakutasaidia kuwachukulia hatua za kisheria wala rushwa. Hivyo wewe mwananchi una jukumu la kuwa tayari kutoa ushahidi wa vitendo vya rushwa ulivyoshuhudia katika Mahakama au popote pale unapohitajika kufanya hivyo.

Kutoa elimu: Mwananchi yeyote una jukumu la kumuelimisha mwananchi mwenzako kuhusiana na suala la rushwa na athari zake kwake yeye na jamii kwa ujumla. Kwa kufanya hivyo utakuwa umesaidia mwananchi huyo kuepuka kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Kuacha rushwa: Mwananchi unatakiwa kuichukia rushwa na kuepuka kushiriki vitendo vya rushwa. Rushwa ni kikwazo kikubwa kwa demokrasia, utawala bora, haki za binadamu na ni tishio kwa amani, utulivu na usalama katika jamii. Wewe ndiye unayeathirika zaidi katika kila tendo la rushwa unaloshiriki, hivyo AMKA, ACHA RUSHWA!

Kutii sheria: Mwananchi, ni lazima uishi kwa kutii sheria, kanuni na taratibu za nchi pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali za kuzuia na kupambana na rushwa. Mwananchi unatakiwa kubadili mawazo na mtazamo kwamba mapambano dhidi ya rushwa ni ya TAKUKURU au vyombo fulani peke yake

HISTORIA YA TAASISI

edit

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya Mwaka 2007. Sheria hii ilitungwa baada ya kufutwa kwa Sheria ya Kuzuia Rushwa (TAKURU) Sura ya 329 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002. Kuanzishwa kwa chombo hiki kulikuja baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha Mswada wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wa mwaka 2007 mnamo tarehe 16 Aprili, 2007. Mswada huu ulisainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete kuwa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mnamo tarehe 11 Juni, 2007 na ilianza kufanya kazi tarehe 1 Julai, 2007.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), pamoja na mambo mengine, ina jukumu la kuzuia rushwa kupitia uimarishaji mifumo.Aitha kwenye moja ya majarada maarufu kama mwananchi imeelezea taasisi nne vinara wa rushwa[4] huku Jeshi la Polisi likishika nafasi ya kwanza kwa asilimia 45.6 kati ya nne vinara.Taasisi nyingine ni zile za afya asilimia 17.9, Mahakama ikishika nafasi ya tatu kwa asilimia 11.9 na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) nafasi ya nne, ikiwa na asilimia 6.1 ikionyesha mwingiliano wa karibu kati yake na sekta ya biashara.Katika utafiti wa mwaka 2020 umeonyesha waathirika wanaokutana na vitendo hivyo katika sekta ya afya, wanawake walikuwa na uwezekano mkubwa wa kutoa hongo(asilimia 4.8 ikilinganishwa na asilimia 3.1 kwa wanaume) katika kutafuta huduma za afya kwa ajili yao wenyewe au za watoto

References

edit
  1. ^ "Rushwa", Wikipedia, kamusi elezo huru (in Swahili), 2020-05-02, retrieved 2024-04-16
  2. ^ "Aina kadhaa za rushwa,hata wanaojifanya kupinga rushwa,wanatoa rushwa". JamiiForums. 2020-12-08. Retrieved 2024-04-16.
  3. ^ "Jinsi ya kushiriki katika kupambana na rushwa". JamiiForums. 2021-01-25. Retrieved 2024-04-16.
  4. ^ "Takukuru yataja taasisi nne vinara wa rushwa". Mwananchi. 2022-10-14. Retrieved 2024-04-16.