Kevin Lameck (amezaliwa tar.24 may 1993 mjini Moshi mkoani Kilimanjaro) ni mtangazaji,mwandishi na mwandaaji wa vipindi vya redio na Televisheni nchini Tanzania.Kevin amebobea kwenye ufanyaji wa vipindi vya siasa na kijamii na amejipata kwenye nafasi ya kufanya aswa vipindi vya asubuhi na jioni kwenye redio mbalimbali nchini na baadaye kama mtunzi na mwandaaji wa vipindi mbalimbali huku ndoto kuu aliyonayo ikiwa ni kufika mbali zaidi kupitia tasnia ya habari nchini Tanzania.

MAFUNZO

edit

Kevin alisoma Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha kwa miaka mitatu kuanzia march 2011 hadi mwaka 2014 na baadaye kusoma kozi kadhaa zenye nia ya kukuza ujuzi juu ya uandishi wa habari,uandaaji wa vipindi na utangazaji sambamba na uandishi wa habari za kiuchunguzi.

ASILI

edit

Amezaliwa 24 May 1993 katika kijiji cha Uduru, kata ya Machame, , jimbo la uchaguzi la Hai, Wilaya ya Hai, mkoa wa Kilimanjaro.

Lugha ya mama ilikuwa Kichaga.

Alizaliwa katika familia ya wakulima na wafanyabiashara.

FAMILIA

edit

Alizaliwa kati ya watoto wanne wa familia yake huko kaskazini mwa Tanzania. Baba alikuwa mfanyabiashara. alifuata mfumo wote wa elimu ya Tanzania akiwa kaskazini mwa Tanznaia. Alipofikia umri wa miaka 19 alipelekwa kama mwanafunzi kwaajili ya masomo yake ya aelimu ya juu mkoani Arusha.

KAZI

edit

Kevin kwa mujibu wa rekodi mbalimbali za ufanyaji kazi wake inaelezwa kuwa alianzia kazi yake mashariki mwa nchi jijini dar es salaam kabla ya kuelekea mkoani Iringa kwenye kituo cha redio country fm alipohudumu kwa miaka miwili,na baadaye kueleka Njombe kwenye kituo cha redio Uplands fm alipohudumu kwa muda mfupi zaidi wa miezi mitano na baadaye kuelekea kwenye kituo cha sasa cha redio Ebony fm-nyanda za juu kusini mwa Tanzania.