Jioni hii kumetokea ajali ya gari ya polisi aina ya defender Mbeya iliokuwa ikipeleka askari wa FFU lindoni

wamefariki 2 na majeruhi 9.

Ajali ya gari kuacha njia kupinduka na kusababisha vifo na majeruhi -

Mnamo tarehe 18.01.2018 majira ya saa 16:45 hrs huko maeneo ya Iwambi barabara ya Mbeya Tunduma kata ya Iwambi tarafa ya Iyunga jiji na Mkoa wa Mbeya gari no PT.2079 Landrover mali ya Jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Mbeya likiendeshwa na askari no. G.3452 PC Adam miaka 30, wakati likiwa linapeleka askari kazini iliacha njia na kupinduka na kusababisha vifo vya askari wawili.

#ngomboziMEDIANEWS