Andrew Carlos (alizaliwa 26 Aprili 1984)[1] ni mwandishi na mhariri kutoka Tanzania, mwandishi wa vitabu, mdau wa muziki, mbunifu wa mavazi, muigizaji, mtunzi wa script katika filamu. [2] Anafanya kazi katika kampuni kubwa ya kuzalisha magazeti pendwa inayojulikana kama Global Publishers yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam.

Andrew alianza kipaji chake cha uandishi nchini Tanzania na miongoni mwa magazeti anayoyaandikia ni pamoja Risasi Mchanganyiko, Amani, Uwazi, Championi, Risasi Jumamosi, Ijumaa pamoja na Ijumaa Wikienda.

MWaka 2016, alikuwa mhariri msaidizi katika Gazeti la Amani na mwaka 2017 akawa mhariri katika Gazeti la Ijumaa linalotoka kila siku ya Ijumaa likiwa na kurasa 24 ambalo ni gazeti lenye kurasa nyingi kupita magazeti pendwa yote nchini Tanzania.